MASOMO YA MISA, MACHI 17, 2022: ALHAMISI, JUMA LA 2 LA KWARESIMA

✍️ DIN - Melkisedeck Leon ShineπŸ“… 2022-03-16 19:25:08πŸ’¬ 50 comments⏱️ ~3 min read
πŸ“„ PDF

SOMO 1

Yer. 17:5-10

Bwana asema hivi: Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake, na moyoni mwake amemwacha Bwana. Maana atakuwa kama fukara nyikani, hataona yatakapotokea mema; bali atakaa jangwani palipo na ukame, katika nchi ya chumvi isiyokaliwa na watu. Amebarikiwa mtu yule anayemtegemea Bwana, ambaye Bwana ni tumaini lake. Maana atakuwa kama mti uliopandwa kando ya maji, uenezao mizizi yake karibu na mto; hautaona hofu wakati wa hari ujapo, bali jani lake litakuwa bichi; wala hautahangaika mwaka wa uchache wa mvua, wala hautaacha kuzaa matunda. Moyo huwa mdanganyifu kuliko vitu vyote, una ugonjwa wa kufisha; nani awezaye kuujua? Mimi, Bwana, nauchunguza moyo, navijaribu viuno, hata kumpa kila mtu kiasi cha njia zake, kiasi cha matunda ya matendo yake. Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATIKATI

Zab. 1:1-4, 6 (K) 40:4

(K) Heri aliyemfanya Bwana kuwa tumaini lake. Heri mtu yule asiyekwenda Katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia ya wakosaji; Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha. Bali sheria ya Bwana ndiyo impendezayo, Na sheria yake huitafakari mchana na usiku. (K) Naye atakuwa kama mti uliopandwa Kandokando ya vijito vya maji, Uzaao matunda yake kwa majira yake, Wala jani lake halinyauki; Na kila alitendalo litafanikiwa. (K) Sivyo walivyo wasio haki; Hao ni kama makapi yapeperushwayo na upepo. Kw akuwa Bwana anaijua njia ya wenye haki, Bali njia ya wasio haki itapotea. (K)

SHANGILIO

Nitaondoka, nitakwenda kwa baba yangu na kumwambia, Baba, nimekosa juu ya mbingu na mbele yako.

INJILI

Lk. 16:19-31

Yesu aliwaambia Mafarisayo: Palikuwa na mtu mmoja, tajiri, aliyevaa nguo za rangi ya zambarau na kitani safi, na kula sikuzote kwa anasa. Na maskini mmoja, jina lake Lazaro, huwekwa mlangoni pake, ana vidonda vingi, naye alikuwa akitamani kushibishwa kwa makombo yaliyoanguka katika meza ya yule tajiri; hata mbwa wakaja wakamramba vidonda vyake. Ikawa yule maskini alikufa, akachukuliwa na malaika mpaka kifuani kwa Ibrahimu. Yule tajiri naye akafa, akazikwa. Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Ibrahimu kwa mbali, na Lazaro kifuani mwake. Akalia, akasema, Ee baba Ibrahimu, nihurumie, umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini, auburudishe ulimi wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu. Ibrahimu akasema, Mwanangu, kumbuka ya kwamba wewe uliyapokea mambo mema yako katika maisha yako, na Lazaro vivyo alipata mabaya; na sasa yeye yupo hapa anafarijiwa, na wewe unaumizwa. Na zaidi ya hayo, kati yetu sisi na ninyi kumewekwa shimo kubwa, ili wale watakao kutoka huku kwenda kwenu wasiweze; wala watu wa kwenu wasivuke kuja kwetu. Akasema, Basi, baba, nakuomba, umtume nyumbani kwa baba yangu, kwa kuwaninao ndugu watano, ili awashuhudie, wasije wao piawakafika mahali hapa pa mateso. Ibrahimu akasema, Wanao Musa na manabii; na wawasikilize wao. Akasema, La, baba Ibrahimu, lakini kama akiwaendea atokaye kwa wafu, watatubu. Akamwambia wasipowasikia Musa na manabii, hawatashawishwa hata mtu akifufuka katika wafu. Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.
πŸ’¬

Discussion

Comments are public to read. Sign in to participate in the discussion.

50 comment(s)
πŸ” Login required to comment or reply

You can read the discussion, but only logged-in AckySHINE users can post comments or replies.

Log in to participate
J
Janet Mwikali2021-01-23 13:36:17
Wacha nuru yako iangaze mbele ya wengine
J
Janet Mwikali2020-11-29 23:08:51
Kupitia Kristo, tunapokea rehema za Mungu kwa wingi
N
Nicholas Wanjohi2020-07-18 13:10:38
Tumeokolewa kwa rehema zake, si kwa matendo yetu
E
Elizabeth Mtei2020-06-20 10:01:38
Rehema hushinda hukumu
S
Samuel Were2020-06-13 10:52:06
Kuna tumaini kwa ajili ya siku zijazo, maana Mungu anajua mipango aliyokupangia
J
Joyce Mussa2019-12-24 22:53:00
Sifa kwa Bwana!
S
Stephen Amollo2019-04-17 01:31:46
Katika giza, nuru yake inaangaza zaidi
J
James Kawawa2019-04-16 21:08:13
Mungu ni kimbilio letu na nguvu zetu, siku zote tayari kusaidia wakati wa shida
G
Grace Mushi2019-02-17 11:56:06
Ahadi za Mungu ni za kweli daima
J
James Malima2018-12-18 20:27:50
Bwana atapigana kwa ajili yako; wewe unahitaji tu kutulia
M
Mercy Atieno2018-11-25 06:43:17
Endelea kuwa na imani!
S
Simon Kiprono2018-01-22 03:54:34
Mwamini Bwana kwa moyo wako wote, na usitegemee ufahamu wako mwenyewe
F
Faith Kariuki2017-11-29 11:33:40
Katika uwepo wake, kuna ukamilifu wa furaha
C
Charles Mchome2017-09-11 01:17:18
Mungu ana kusudi hata katika maumivu yako
J
Joseph Kawawa2017-06-22 10:17:27
Katika rehema zake, Mungu husamehe na kurejesha
P
Paul Kamau2017-06-13 10:35:34
Hauko peke yako; Mungu yuko nawe
G
Grace Minja2017-05-10 01:31:11
Tembea kwa imani, si kwa kuona
J
Joyce Nkya2017-03-19 17:40:49
Bwana yuko karibu na wote wanaomwita
V
Victor Malima2017-01-03 00:27:33
Mungu ana mpango kwa ajili yako, muamini
V
Victor Sokoine2016-10-24 05:48:49
Endelea kuamini, hata ikiwa ni vigumu kuona njia