ACKYSHINE ARTICLE Β· PRINTABLE READER

Je, kuharibika mimba kunasababishwa na nini?

✍️ SW - Melkisedeck ShineπŸ“… April 17, 2022πŸ’¬ 0 comments
πŸ—‚οΈ Ujana na Makuzi | Mapenzi na Ngono Salama🌐 Kiswahili
Je, kuharibika mimba kunasababishwa na nini?
Asimilia kumi hadi i i ishirini ya mimba huharibika. Mimba nyingi zinaharibika katika kipindi cha wiki 12 za mwanzo wa ujauzito. Sababu kuu hutokana na kuharibika kwa yai lililotungwa mimba. Iwapo yai lingeendelea kukua katika hali hii matokeo ni mtoto kuzaliwa na kasoro mwilini au kiakili. Kwa hiyo mimba kuharibika inaweza kuwa ni njia ya asili ya mwili kukabiliana na matatizo hayo ya kimaumbile. Vilevile kuharibika kwa mimba huweza kutokea kama mama ana magonjwa kama malaria au kaswende, kama ameanguka chini kwa nguvu au kama ana matatizo kwenye via vya uzazi. Dalili za mimba kuharibika ni damu kutoka ukeni na maumivu makali ya tumbo kwa chini.
βœ…
Direct PDF download

The download button now generates the PDF on the server. It no longer depends on an off-screen browser canvas, so the former blank-PDF capture path is bypassed.