Uhusiano mzuri na wazazi ni muhimu sana siyo katika masuala ya uchaguzi wa mchumba tu, bali katika masuala yote ya msingi maishani. Kwa hiyo, hatua ya kwanza ni kujaribu kuelewana nao.
Mara nyingi vijana hufikiri wazazi hawaelewi maisha ya vijana wa kisasa. Mara nyingine hufikiri kwamba mila na desturi zinamzuia kijana kufanya uamuzi ambao unafaa. Pia wengine hufikiri kwamba tofauti ya malengo kati ya vijana na wazazi huleta mgongano.
Hali kama hii ikijitokeza, ni vizuri kuwasiliana na wazazi kwa nia ya kuelewana. Usisahau kwamba wazazi wakati wote wanajaribu kujena maisha bora ya baadaye ya watoto wao. Unapowasiliana na wazazi jaribu kuwaeleza kwa heshima na upole kwa nini hukubaliani na mawazo yao na kwa nini unaona uamuzi wako unafaa. Inawezekana kwa kufanya hivi unaweza kupata ridhaa ya wazazi wako.
Kama hujawahi kuzungumza na wazazi wako kwa karibu, mara nyingi i i inakuwa vigumu kuanzisha mazungumzo. Jaribu kuanza kwa mazungumzo rahisi. Tafuta muda mzuri wa kuanzisha mazungumzo. Usianzishe mazungumzo na wazazi wakati wamechoka au wakati wametingwa na kazi nyingi; hawatakusikiliza. Jaribu kuwa wazi na mkweli, na waonyeshe wazazi wako kwamba unayajali mawazo yao. Kwa kufanya hivyo wazazi wako wanaweza kukuamini na kuafikiana na wewe katika maswali mazito zaidi. Vilevile onyesha kwamba unawaheshimu. Inachukua muda mrefu kufanikisha mawasiliano mazuri na wazazi, lakini ni vema kuyaanzisha mapema kwa ajili ya kufanikisha lengo la mawasiliano mazuri na wazazi.
Uhusiano mzuri na wazazi ni muhimu sana siyo katika masuala ya uchaguzi wa mchumba tu, bali katika masuala yote ya msingi maishani. Kwa hiyo, hatua ya kwanza ni kujaribu kuelewana nao. Mara nyingi vijana hufikiri wazazi hawaelewi maisha ya vijana wa kisasa. Mara nyingine hufikiri kwamba mila na desturi zinamzuia kijana kufanya uamuzi ambao unafaa. Pia wengine hufikiri kwamba tofauti ya malengo kati ya vijana na wazazi huleta mgongano. Hali kama hii ikijitokeza, ni vizuri kuwasiliana na wazazi kwa nia ya kuelewana. Usisahau kwamba wazazi wakati wote wanajaribu kujena maisha bora ya baadaye ya watoto wao. Unapowasiliana na wazazi jaribu kuwaeleza kwa heshima na upole kwa nini hukubaliani na mawazo yao na kwa nini unaona uamuzi wako unafaa. Inawezekana kwa kufanya hivi unaweza kupata ridhaa ya wazazi wako. Kama hujawahi kuzungumza na wazazi wako kwa karibu, mara nyingi i i inakuwa vigumu kuanzisha mazungumzo. Jaribu kuanza kwa mazungumzo rahisi. Tafuta muda mzuri wa kuanzisha mazungumzo. Usianzishe mazungumzo na wazazi wakati wamechoka au wakati wametingwa na kazi nyingi; hawatakusikiliza. Jaribu kuwa wazi na mkweli, na waonyeshe wazazi wako kwamba unayajali mawazo yao. Kwa kufanya hivyo wazazi wako wanaweza kukuamini na kuafikiana na wewe katika maswali mazito zaidi. Vilevile onyesha kwamba unawaheshimu. Inachukua muda mrefu kufanikisha mawasiliano mazuri na wazazi, lakini ni vema kuyaanzisha mapema kwa ajili ya kufanikisha lengo la mawasiliano mazuri na wazazi.
π¬
Discussion
Comments are public to read. Sign in to participate in the discussion.
0 comment(s)
π Login required to comment or reply
You can read the discussion, but only logged-in AckySHINE users can post comments or replies.
Je, kuna tofauti za kiutamaduni katika ngono/kufanya mapenzi? Swali hili linaweza kusababisha majibu tofauti kutoka kwa watu tofauti. Hata hivyo, ni mβ¦
Pombe huingia kwenye damu na kuzunguka mwili mzima pamojana kwenye ubongo wako. Ina madhara kwa viungo vya mwiliwako na ubongo wako na hivyo huathiri β¦
Ngozi ya Albino haina jinsi ya kujilinda na mionzi ya jua. Inaunguasana baada ya kupatwa na jua na ngozi huwasha na kuuma. Ngoziya Albino inajitahidi β¦
Ndiyo, i inawezekana kwamba mwanamke anayepata hedhi yake kila mwezi akawa mgumba. Na vilevile i inawezekana kwamba mwanamke asiyepata hedhi kila mwezβ¦
Wakati mwingine, migogoro katika uhusiano wako na msichana inaweza kuonekana kama jambo lisiloweza kutatuliwa. Lakini kuna njia za kusuluhisha migogorβ¦
Kwa nini Ni Lazima Kufanya Ngono na Mtu Mmoja Tu? π Habari za leo vijana wangu! Leo tutaongelea suala muhimu sana katika maisha yetu ya kimapenzi. Kwaβ¦
Discussion
Comments are public to read. Sign in to participate in the discussion.
You can read the discussion, but only logged-in AckySHINE users can post comments or replies.
Log in to participate