Tofauti ya VVU na UKIMWI

✍️ SW - Melkisedeck ShineπŸ“… 2022-04-17 03:31:17πŸ’¬ 1 comments⏱️ ~1 min read
πŸ“„ PDF
Neno VVU ni i virusi au vijidudu vinavyosababisha ugonjwa wa UKIMWI. Neno hili kwa lugha ya Kii ngereza ni HIV yaani β€œHuman Immunodeficiency Virus”. UKIMWI ni kifupi cha maneno matatu ambayo ni Upungufu wa Kinga Mwilini. Kwa Kii ngereza jina la UKIMWI AIDS ambacho kirefu chake ni β€œAcquired Immune Deficiency Syndrome”. Neno UKIMWI tayari linaonyesha tayari aina ya ugonjwa, i ikii manisha kuwa mwili umepungua uwezo wake wa kinga kwa maradhi mbalimbali mwilini. Dalili za upungufu huu ukianza kujitokeza basi maradhi haya huitwa UKIMWI. Tofauti kati ya VVU na UKIMWI ni kuwa mtu aliyeambukizwa VVU bado anaweza kuonekana mzima wa afya. Pamoja na kuwa virusi hivyo vitaonenekana katika damu yake, ni kwamba virusi hivyo vitakuwa havijaanza bado kushambulia chembechembe nyeupe za damu. Kwa upande mwingine kinga ya mwili ya mtu anayeumwa UKIMWI i itakuwa tayari i i imepungua. Mwili wake utaanza kuugua magonjwa nyemelezi. Magonjwa nyemelezi hupata nafasi ya kushambulia mwili huu ambao tayari kinga imepungua. Watu wnaoumwa UKIMWI wanaweza kupungua uzito wa mwili, kuharisha au kupata matatizo ya ngozi. Hata hivyo maradhi haya siyo lazima yatokane na kuwa na VVU. Ili kuwa na uhakika, onana na mtaalamu yaani dakatari wako.
πŸ’¬

Discussion

Comments are public to read. Sign in to participate in the discussion.

1 comment(s)
πŸ” Login required to comment or reply

You can read the discussion, but only logged-in AckySHINE users can post comments or replies.

Log in to participate
B
Beno2026-04-17 18:30:20 Β· User
Ujasiri ndo mchawi