Upungufu wa maji ni pale mwili unapopoteza kiasi kingi cha maji kwa njia mbalimbali, ikiwemo jasho na mkojo, mwili hupungukiwa maji na hivyo mtu huyo huambiwa ana upungufu wa maji. Tunaelezwa kuwa karibu theluthi mbili ya miili yetu imejaa maji.
Ili mwili uweze kufanya kazi yake vizuri, kiwango cha maji mwilini hakipaswi kupungua hata kidogo, hivyo kila mtu ana wajibu wa kunywa maji ya kutosha kila siku ili kulinda kiwago chake cha maji kisipungue na kinapopungua ndipo hapo mwili huanza kuonesha dalili za kukaukiwa maji (dehydration).
Zifutazo ndizo dalili za upungufu wa maji mwilini;
Dalili za upungufu wa maji kwa mtoto.
Kwa kawaida, dalili za upungufu wa maji mwilini hujitokeza zaidi kwa watoto wadogo kuliko watu wazima au wazee. Dalili za upungufu wa maji mwilini kwa watoto huweza kusabababishwa ama na kuharisha, kutapika, kutokunywa maji au vimiminika vingine vya kutosha.
Mtoto mwenye dalili za upungufu wa maji huweza kuonesha dalili zifutazo:
Kukojoa mara chache sana
Mdomo na ulimi kukauka
Mtoto kulia mara kwa mara na anapolia machozi hayatoki.
Mtoto kutokuwa mchangamfu
Macho, tumbo au mashavu kubonyea
Dalili za upungufu wa maji kwa wazee.
Dalili za upungufu wa maji kwa wazee ni tofauti na watu wazima. Wazee wa umri zaidi ya miaka 60 huwa na ngozi iliyosinyaa na hata ukiiminya, hubaki katika hali hiyo kwa muda na unapoikwaruza alama hubaki.
Halikadhalika, wazee hukosa haja ndogo kwa muda mrefu, hupungukiwa uzito kwa kiasi kikubwa na hupatwa na homa.
Dalili za upungufu wa maji kwa wajazito.
Upungufu wa maji mwilini kwa waja wazito ni hatari kwa mama pamoja na mtoto. Dalili zinazoweza kujitokeza kwa waja wazito ni pamoja na:
Kukojoa mkojo wa njano nyeusi
Kuumwa na kichwa.
Mwili kukosa nguvu.
Kichefuchefu na kutapika.
Kukaukwa na mdomo.
Ili kujiepusha na matatizo ya upungufu wa maji na hatimaye kujikuta unakumbwa na dalili kadhaa zilizoelezewa hapo, ambazo ziko pia kwa watu wazima wengine, ni kuwa na mazoea ya kunywa maji ya kutosha kila siku. Hata utakapozidiwa na kukimbizwa hospitali, hakuna dawa nyingine utakayopewa zaidi ya maji (re-hydrating solution) . Kwa nini usubiri hali hiyo ikutokee wakati unaweza kuizuia kwa kunywa maji tu?
Hivyo wito wetu kwako kuendelea kunywa maji mengi ya kutosha kadri uwezavyo hii itakusaidia sana kwa namna moja ama nyingine kuwa na afya bora
Upungufu wa maji ni pale mwili unapopoteza kiasi kingi cha maji kwa njia mbalimbali, ikiwemo jasho na mkojo, mwili hupungukiwa maji na hivyo mtu huyo huambiwa ana upungufu wa maji. Tunaelezwa kuwa karibu theluthi mbili ya miili yetu imejaa maji. Ili mwili uweze kufanya kazi yake vizuri, kiwango cha maji mwilini hakipaswi kupungua hata kidogo, hivyo kila mtu ana wajibu wa kunywa maji ya kutosha kila siku ili kulinda kiwago chake cha maji kisipungue na kinapopungua ndipo hapo mwili huanza kuonesha dalili za kukaukiwa maji (dehydration). Zifutazo ndizo dalili za upungufu wa maji mwilini; Dalili za upungufu wa maji kwa mtoto. Kwa kawaida, dalili za upungufu wa maji mwilini hujitokeza zaidi kwa watoto wadogo kuliko watu wazima au wazee. Dalili za upungufu wa maji mwilini kwa watoto huweza kusabababishwa ama na kuharisha, kutapika, kutokunywa maji au vimiminika vingine vya kutosha. Mtoto mwenye dalili za upungufu wa maji huweza kuonesha dalili zifutazo: Kukojoa mara chache sana Mdomo na ulimi kukauka Mtoto kulia mara kwa mara na anapolia machozi hayatoki. Mtoto kutokuwa mchangamfu Macho, tumbo au mashavu kubonyea Dalili za upungufu wa maji kwa wazee. Dalili za upungufu wa maji kwa wazee ni tofauti na watu wazima. Wazee wa umri zaidi ya miaka 60 huwa na ngozi iliyosinyaa na hata ukiiminya, hubaki katika hali hiyo kwa muda na unapoikwaruza alama hubaki. Halikadhalika, wazee hukosa haja ndogo kwa muda mrefu, hupungukiwa uzito kwa kiasi kikubwa na hupatwa na homa. Dalili za upungufu wa maji kwa wajazito. Upungufu wa maji mwilini kwa waja wazito ni hatari kwa mama pamoja na mtoto. Dalili zinazoweza kujitokeza kwa waja wazito ni pamoja na: Kukojoa mkojo wa njano nyeusi Kuumwa na kichwa. Mwili kukosa nguvu. Kichefuchefu na kutapika. Kukaukwa na mdomo. Ili kujiepusha na matatizo ya upungufu wa maji na hatimaye kujikuta unakumbwa na dalili kadhaa zilizoelezewa hapo, ambazo ziko pia kwa watu wazima wengine, ni kuwa na mazoea ya kunywa maji ya kutosha kila siku. Hata utakapozidiwa na kukimbizwa hospitali, hakuna dawa nyingine utakayopewa zaidi ya maji (re-hydrating solution) . Kwa nini usubiri hali hiyo ikutokee wakati unaweza kuizuia kwa kunywa maji tu? Hivyo wito wetu kwako kuendelea kunywa maji mengi ya kutosha kadri uwezavyo hii itakusaidia sana kwa namna moja ama nyingine kuwa na afya bora
π¬
Discussion
Comments are public to read. Sign in to participate in the discussion.
0 comment(s)
π Login required to comment or reply
You can read the discussion, but only logged-in AckySHINE users can post comments or replies.
Hii ni mbegu bora inaitwa UPENDO ipande kwa ndg zako,na pale utakapokuta imeota imwagilie maji ya FURAHA,iwekee kivuli cha USHIRIKIANO, ipalilie kwa jβ¦
Unahitaji vitu vifuatavyo:a)Binzari ya ungab)Maziwa freshc)Asalid)Bakulie)Kijiko cha chaiHatua kwa hatua namna ya kutumia:a)Weka kijiko kidogo kimoja β¦
Nakupenda mpenzi wangu, sifikirii kitu chochote zaidi yakona kwa kuwa nakupenda sipendi kuwa na urafiki hata namwingine kwani atakuwa anabana nafasi nβ¦
β‘ Asubuhi saa 12 : 00 mtu anaamka, kabla hata HAJAMUSHUKURU MUNGU, kabla hata hajatoka kitandani, kabla hata hajajifunua shuka,πATARIPOTI KWA SIMU KWAβ¦
Discussion
Comments are public to read. Sign in to participate in the discussion.
You can read the discussion, but only logged-in AckySHINE users can post comments or replies.
Log in to participate