Faida za matumizi ya Ukwaju kiafya

✍️ SW - Melkisedeck ShineπŸ“… 2022-04-15 04:06:13πŸ’¬ 0 comments⏱️ ~1 min read
πŸ“„ PDF

Faida kuu za ukwaju ni kama ifuatavyo:

Huondoa sumu Mwilini

Chanzo kizuri cha viua sumu mwilini 'antioxidants' ambavyo huzuia Saratani (cancer)

Una Vitamin B na C

Chanzo cha Vitamini B na C vile vile "carotentes"

Huondoa homa

Hushusha joto la mwili na kuondosha homa, hasa homa ya malaria na homa ya matumbo

Huzuia mafua

Huulinda mwili dhidi ya mafua na kero za mafua kooni

Husaidia mmengenyo wa chakula

Husaidia myeyusho na mmengenyo wa chakula na kuondosha kuvimbiwa

Hutibu nyongo

Husaidia kutibu matatizo ya nyongo (bile disorders)

Husaidia kurahisisha choo (laxative)

Hupunvuza Lehemu

Husaidia kupunguza wingi wa lehemu (cholesterol) na hivyo kuimarisha moyo

Husaidia Ngozi

Husaidia ngozi kuwa nyororo, vile vile husaidia ngozi inayopona baada ya kuungua au yenye vidonda

Huua minyoo

Husaidia kuua minyoo tumboni (kwa watoto wadogo

πŸ’¬

Discussion

Comments are public to read. Sign in to participate in the discussion.

0 comment(s)
πŸ” Login required to comment or reply

You can read the discussion, but only logged-in AckySHINE users can post comments or replies.

Log in to participate
No comments yet.