Mwongozo wa namna ya Kusali Rozari Takatifu ya Mama Bikira Maria
Anza kusali Rozari kwa kuibusu miguu ya Bwana Yesu katika taswira (picha) yake Msalabani kisha fanya Ishara ya Msalaba ukiwa unasema “Kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu, Amina”.
Taja kwa ufupi nia za Rozari hii. Tangaza nia hizo kwa sauti kama mnasali wengi kwa pamoja, Mfano, “Tusali kuombea amani katika nchi yetu na ulimwenguni kote, na tuunganishe nia hizo na nia zetu sisi wenyewe, nk).
Baada ya Sala ya Nasadiki pamoja na ya Baba Yetu, tunamwomba Mungu (Utatu Mtakatifu) fadhila za Imani, Matumaini na Mapendo, zikiambatana na Salamu Maria tatu.
Mojawapo ya maneno yafuatayo huweza kutumika: “Mungu Baba utuongezee Imani. Salamu Maria, …… Mungu Mwana utuongezee matumaini, Salamu Maria, …… Mungu Roho Mtakatifu washa nyoyo zetu kwa mapendo yako, Salamu Maria, …..”
Au;
“Utuongezee Imani ee Bwana, Salamu Maria,…. Utuongezee matumaini ee Bwana, Salamu Maria,…. Uwashe nyoyo zetu kwa mapendo yako ee Bwana, Salamu Maria, …..” Au; “Salamu e uliyechaguliwa na Mungu Baba, Salamu Maria,….. Salamu e Mama wa Mungu Mwana, Salamu Maria,….. Salamu e Mchumba wa Mungu Roho Mtakatifu, Salamu Maria,……” Atukuzwe Baba, na Mwana na Roho Mtakatifu, kama mwanzo na sasa na siku zote, na milele, Amina.
Ee Yesu wangu, utusamehe dhambi zetu, utuepushe na moto wa milele, ongoza roho zote mbinguni, hasa za wale wanaohitaji huruma yako zaidi. Tuwasifu milele, Yesu, Maria na Yosef.
Kisha endelea na sala zinazofuata kama mpangilio unavyoonyesha hapo juu.
Kila baada ya Tendo moja na makumi ya Salamu Maria…, “Atukuzwe..”, “Ee Yesu wangu…” na “Tuwasifu milele…” kama muda unatosha wimbo ufaao wa Bikira Maria uimbwe (kama muda ni mfupi basi angalau ubeti mmoja mmoja uimbwe kila baada ya makumi hayo). Baada ya Wimbo, Tendo linalofuata litangazwe kwa sauti pamoja na tafakari fupi au ombi linaloambatana na Tendo husika kama inavyoonyeshwa hapa chini.
MATENDO YA ROZARI TAKATIFU
MATENDO YA FURAHA (Jumatatu na Jumamosi)
Tendo la kwanza; Malaika Gabrieli anampasha habari Maria kuwa atakuwa Mama wa Mungu. Tumwombe Mungu atujalie unyenyekevu.
Tendo la pili; Maria Mtakatifu anakwenda kumtembelea Elizabeti. Tumwombe Mungu atujalie mapendo ya jirani.
Tendo la tatu; Yesu anazaliwa Betlehemu. Tumwombe Mungu atujalie moyo wa ufukara
Tendo la nne; Yesu anatolewa hekaluni. Tumwombe Mungu atujalie usafi wa moyo.
Tendo la tano; Maria anamkuta Yesu hekaluni. Tumwombe Mungu atujalie kuwatii wakubwa wetu.
MATENDO YA UCHUNGU (Jumanne na Ijumaa)
Tendo la kwanza; Yesu anatoka jasho la damu kwa ajili yetu. Tumwombe Mungu atujalie sikitiko la dhambi.
Tendo la pili; Yesu anapigwa kwa mijeledi kwa ajili yetu. Tumwombe Mungu atujalie kuacha dhambi za uchafu.
Tendo la tatu; Yesu anatiwa miiba kichwani kwa ajili yetu. Tumwombe Mungu atujalie kushinda kiburi.
Tendo la nne; Yesu anachukua Msalaba kwa ajili yetu. Tumwombe Mungu atujalie kuvumilia taabu.
Tendo la tano; Yesu anakufa Msalabani. Tumwombe Mungu atujalie kuwapenda Yesu na Maria.
MATENDO YA UTUKUFU (Jumatano na Jumapili)
Tendo la kwanza; Yesu anafufuka. Tumwombe Mungu atujalie kugeuka watakatifu.
Tendo la pili; Yesu anapaa mbinguni. Tumwombe Mungu atujalie kwenda mbinguni.
Tendo la tatu; Roho Mtakatifu anawashukia Mitume. Tumwombe Mungu atujalie bidii katika dini yetu.
Tendo la nne; Bikira Maria anapalizwa mbinguni. Tumwombe Mungu atujalie kufa vizuri.
Tendo la tano; Bikira Maria anawekwa Malkia mbinguni. Tumwombe Mungu atujalie kudumu katika njia njema.
MATENDO YA MWANGA (Alhamisi)
Tendo la kwanza; Yesu anabatizwa Mto Jordani. Tumwombe Mungu atujalie uaminifu kwa ahadi zetu za ubatizo.
Tendo la pili; Yesu anageuza maji kuwa divai huko Kana. Tumwombe Mungu atujalie kuukoleza ulimwengu kwa chachu ya enjili.
Tendo la tatu; Yesu anatangaza Ufalme wa Mungu. Tumwombe Mungu atujalie kupokea Ufalme wake kwa toba ya kweli.
Tendo la nne; Yesu anageuka sura. Tumwombe Mungu atujalie neema ya kuung’arisha ulimwengu kwa uso wa Yesu.
Tendo la tano; Yesu anaweka Sakramenti ya Ekaristia. Tumwombe Mungu atujalie neema ya kujitoa sadaka kwa ajili ya wengine.
LITANIA YA BIKIRA MARIA
Bwana utuhurumie
Bwana utuhurumie
Kristo utuhurumie
Bwana utuhurumie
Bwana utuhurumie
Kristo utusikie
Kristo utusikilize
Mungu Baba wa Mbinguni,…… Utuhurumie
Mungu Mwana Mkombozi wa dunia ……… Utuhurumie
Mungu Roho Mtakatifu …….. Utuhurumie
Utatu Mtakatifu Mungu Mmoja …….. Utuhurumie
Maria Mtakatifu ………. utuombee
Mzazi Mtakatifu wa Mungu …….. utuombee
Bikira Mtakatifu Mkuu wa Mabikira …….. utuombee
Mama wa Kristo ……… utuombee
Mama wa Neema ya Mungu ………….. utuombee
Mama Mtakatifu sana ……… utuombee
Mama mwenye usafi wa Moyo ……….. utuombee
Mama mwenye ubikira ……….. utuombee
Mama usiye na doa ……….. utuombee
Mama mpendelevu ………. utuombee
Mama mstajabivu ………. utuombee
Mama wa Muumba ………. utuombee
Mama wa Mkombozi ………….. utuombee
Mama wa Kanisa……….. utuombee
Bikira mwenye utaratibu ………….. utuombee
Bikira mwenye heshima ………….. utuombee
Bikira mwenye sifa ………….. utuombee
Bikira mwenye uwezo ………….. utuombee
Bikra mweye huruma ………….. utuombee
Bikra mwaminifu………….. utuombee
Kioo cha haki ………….. utuombee
Kikao cha hekima ………….. utuombee
Sababu ya furaha yetu ………….. utuombee
Chombo cha neema ………….. utuombee
Chombo cha kuheshimiwa ………….. utuombee
Chombo bora cha ibada ………….. utuombee
Waridi lenye fumbo ………….. utuombee
Mnara wa Daudi ………….. utuombee
Mnara wa pembe ………….. utuombee
Nyumba ya dhahabu ………….. utuombee
Sanduku la Agano ………….. utuombee
Mlango wa Mbingu ………….. utuombee
Nyota ya asubuhi ………….. utuombee
Afya ya wagonjwa ………….. utuombee
Kimbilio la wakosefu ………….. utuombee
Mtuliza wenye huzuni ………….. utuombee
Msaada wa waKristo ………….. utuombee
Malkia wa Malaika ………….. utuombee
Malkia wa Mababu ………….. utuombee
Malkia wa Manabii ………….. utuombee
Malkia wa Mitume ………….. utuombee
Malkia wa Mashahidi ………….. utuombee
Malkia wa Waungama dini ………….. utuombee
Malkia wa Mabikira ………….. utuombee
Malkia wa Watakatifu wote ………….. utuombee
Malkia uliyepalizwa Mbinguni ………….. utuombee
Malkia wa Rozari takatifu ………….. utuombee
Malkia wa amani ………….. utuombee
Mwanakodoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia,…………..Utusamehe ee Bwana.
Mwanakondoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia,…………..Utusikilize ee Bwana
Mwanakondoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia,…………..Utuhurumie.
Utuombee, Mzazi Mtakatifu wa Mungu,…………..Tujaliwe ahadi za Kristo.
Tuombe
Ee Bwana Mungu, utujalie sisi watumishi wako afya ya roho na mwili siku zote; na kwa maombezi matukufu ya Maria Mtakaatifu Bikira daima, tuopolewe na mashaka ya saa, tupate na furaha za milele. Kwa Kristo Bwana wetu, Amina.
Mwongozo wa namna ya Kusali Rozari Takatifu ya Mama Bikira Maria Anza kusali Rozari kwa kuibusu miguu ya Bwana Yesu katika taswira (picha) yake Msalabani kisha fanya Ishara ya Msalaba ukiwa unasema “Kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu, Amina”. Taja kwa ufupi nia za Rozari hii. Tangaza nia hizo kwa sauti kama mnasali wengi kwa pamoja, Mfano, “Tusali kuombea amani katika nchi yetu na ulimwenguni kote, na tuunganishe nia hizo na nia zetu sisi wenyewe, nk). Baada ya Sala ya Nasadiki pamoja na ya Baba Yetu, tunamwomba Mungu (Utatu Mtakatifu) fadhila za Imani, Matumaini na Mapendo, zikiambatana na Salamu Maria tatu. Mojawapo ya maneno yafuatayo huweza kutumika:“Mungu Baba utuongezee Imani. Salamu Maria, …… Mungu Mwana utuongezee matumaini, Salamu Maria, …… Mungu Roho Mtakatifu washa nyoyo zetu kwa mapendo yako, Salamu Maria, …..” Au; “Utuongezee Imani ee Bwana, Salamu Maria,…. Utuongezee matumaini ee Bwana, Salamu Maria,…. Uwashe nyoyo zetu kwa mapendo yako ee Bwana, Salamu Maria, …..” Au;“Salamu e uliyechaguliwa na Mungu Baba, Salamu Maria,….. Salamu e Mama wa Mungu Mwana, Salamu Maria,….. Salamu e Mchumba wa Mungu Roho Mtakatifu, Salamu Maria,……”Atukuzwe Baba, na Mwana na Roho Mtakatifu, kama mwanzo na sasa na siku zote, na milele, Amina. Ee Yesu wangu, utusamehe dhambi zetu, utuepushe na moto wa milele, ongoza roho zote mbinguni, hasa za wale wanaohitaji huruma yako zaidi.Tuwasifu milele, Yesu, Maria na Yosef. Kisha endelea na sala zinazofuata kama mpangilio unavyoonyesha hapo juu. Kila baada ya Tendo moja na makumi ya Salamu Maria…, “Atukuzwe..”, “Ee Yesu wangu…” na “Tuwasifu milele…” kama muda unatosha wimbo ufaao wa Bikira Maria uimbwe (kama muda ni mfupi basi angalau ubeti mmoja mmoja uimbwe kila baada ya makumi hayo). Baada ya Wimbo, Tendo linalofuata litangazwe kwa sauti pamoja na tafakari fupi au ombi linaloambatana na Tendo husika kama inavyoonyeshwa hapa chini. MATENDO YA ROZARI TAKATIFU MATENDO YA FURAHA (Jumatatu na Jumamosi) Tendo la kwanza; Malaika Gabrieli anampasha habari Maria kuwa atakuwa Mama wa Mungu. Tumwombe Mungu atujalie unyenyekevu. Tendo la pili; Maria Mtakatifu anakwenda kumtembelea Elizabeti. Tumwombe Mungu atujalie mapendo ya jirani. Tendo la tatu; Yesu anazaliwa Betlehemu. Tumwombe Mungu atujalie moyo wa ufukara Tendo la nne; Yesu anatolewa hekaluni. Tumwombe Mungu atujalie usafi wa moyo. Tendo la tano; Maria anamkuta Yesu hekaluni. Tumwombe Mungu atujalie kuwatii wakubwa wetu. MATENDO YA UCHUNGU (Jumanne na Ijumaa) Tendo la kwanza; Yesu anatoka jasho la damu kwa ajili yetu. Tumwombe Mungu atujalie sikitiko la dhambi. Tendo la pili; Yesu anapigwa kwa mijeledi kwa ajili yetu. Tumwombe Mungu atujalie kuacha dhambi za uchafu. Tendo la tatu; Yesu anatiwa miiba kichwani kwa ajili yetu. Tumwombe Mungu atujalie kushinda kiburi. Tendo la nne; Yesu anachukua Msalaba kwa ajili yetu. Tumwombe Mungu atujalie kuvumilia taabu. Tendo la tano; Yesu anakufa Msalabani. Tumwombe Mungu atujalie kuwapenda Yesu na Maria. MATENDO YA UTUKUFU (Jumatano na Jumapili) Tendo la kwanza; Yesu anafufuka. Tumwombe Mungu atujalie kugeuka watakatifu. Tendo la pili; Yesu anapaa mbinguni. Tumwombe Mungu atujalie kwenda mbinguni. Tendo la tatu; Roho Mtakatifu anawashukia Mitume. Tumwombe Mungu atujalie bidii katika dini yetu. Tendo la nne; Bikira Maria anapalizwa mbinguni. Tumwombe Mungu atujalie kufa vizuri. Tendo la tano; Bikira Maria anawekwa Malkia mbinguni. Tumwombe Mungu atujalie kudumu katika njia njema. MATENDO YA MWANGA (Alhamisi) Tendo la kwanza; Yesu anabatizwa Mto Jordani. Tumwombe Mungu atujalie uaminifu kwa ahadi zetu za ubatizo. Tendo la pili; Yesu anageuza maji kuwa divai huko Kana. Tumwombe Mungu atujalie kuukoleza ulimwengu kwa chachu ya enjili. Tendo la tatu; Yesu anatangaza Ufalme wa Mungu. Tumwombe Mungu atujalie kupokea Ufalme wake kwa toba ya kweli. Tendo la nne; Yesu anageuka sura. Tumwombe Mungu atujalie neema ya kuung’arisha ulimwengu kwa uso wa Yesu. Tendo la tano; Yesu anaweka Sakramenti ya Ekaristia. Tumwombe Mungu atujalie neema ya kujitoa sadaka kwa ajili ya wengine. LITANIA YA BIKIRA MARIA Bwana utuhurumieBwana utuhurumieKristo utuhurumieBwana utuhurumieBwana utuhurumieKristo utusikieKristo utusikilize Mungu Baba wa Mbinguni,…… UtuhurumieMungu Mwana Mkombozi wa dunia ……… UtuhurumieMungu Roho Mtakatifu …….. UtuhurumieUtatu Mtakatifu Mungu Mmoja …….. Utuhurumie Maria Mtakatifu ………. utuombeeMzazi Mtakatifu wa Mungu …….. utuombeeBikira Mtakatifu Mkuu wa Mabikira …….. utuombee Mama wa Kristo ……… utuombeeMama wa Neema ya Mungu ………….. utuombeeMama Mtakatifu sana ……… utuombeeMama mwenye usafi wa Moyo ……….. utuombeeMama mwenye ubikira ……….. utuombeeMama usiye na doa ……….. utuombeeMama mpendelevu ………. utuombeeMama mstajabivu ………. utuombeeMama wa Muumba ………. utuombeeMama wa Mkombozi ………….. utuombeeMama wa Kanisa……….. utuombee Bikira mwenye utaratibu ………….. utuombeeBikira mwenye heshima ………….. utuombeeBikira mwenye sifa ………….. utuombeeBikira mwenye uwezo ………….. utuombeeBikra mweye huruma ………….. utuombeeBikra mwaminifu………….. utuombee Kioo cha haki ………….. utuombeeKikao cha hekima ………….. utuombeeSababu ya furaha yetu ………….. utuombeeChombo cha neema ………….. utuombeeChombo cha kuheshimiwa ………….. utuombeeChombo bora cha ibada ………….. utuombeeWaridi lenye fumbo ………….. utuombeeMnara wa Daudi ………….. utuombeeMnara wa pembe ………….. utuombeeNyumba ya dhahabu ………….. utuombeeSanduku la Agano ………….. utuombee Mlango wa Mbingu ………….. utuombeeNyota ya asubuhi ………….. utuombeeAfya ya wagonjwa ………….. utuombeeKimbilio la wakosefu ………….. utuombeeMtuliza wenye huzuni ………….. utuombeeMsaada wa waKristo ………….. utuombee Malkia wa Malaika ………….. utuombeeMalkia wa Mababu ………….. utuombeeMalkia wa Manabii ………….. utuombeeMalkia wa Mitume ………….. utuombeeMalkia wa Mashahidi ………….. utuombeeMalkia wa Waungama dini ………….. utuombeeMalkia wa Mabikira ………….. utuombeeMalkia wa Watakatifu wote ………….. utuombeeMalkia uliyepalizwa Mbinguni ………….. utuombeeMalkia wa Rozari takatifu ………….. utuombeeMalkia wa amani ………….. utuombee Mwanakodoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia,…………..Utusamehe ee Bwana.Mwanakondoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia,…………..Utusikilize ee BwanaMwanakondoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia,…………..Utuhurumie. Utuombee, Mzazi Mtakatifu wa Mungu,…………..Tujaliwe ahadi za Kristo. Tuombe Ee Bwana Mungu, utujalie sisi watumishi wako afya ya roho na mwili siku zote; na kwa maombezi matukufu ya Maria Mtakaatifu Bikira daima, tuopolewe na mashaka ya saa, tupate na furaha za milele. Kwa Kristo Bwana wetu, Amina. Karibu Vitatabu vya Kikatoliki [products orderby="rand" columns="4" category="vitabu-vya-dini" limit="20"]
💬
Discussion
Comments are public to read. Sign in to participate in the discussion.
85 comment(s)
🔐 Login required to comment or reply
You can read the discussion, but only logged-in AckySHINE users can post comments or replies.
Mungu wangu,nasadiki maneno yote linalosadiki na linalofundisha kanisa katoliki la Roma;Kwani ndiwe uliyefundisha hayo,wala hudanganyiki,wala hudangan…
Ee Yosef mwenye heri, tunakimbilia kwako, katika masumbuko yetu, na kishaomba shime ya Mchumba wako Mtakatifu, tunaomba pia kwa matumaini usimamizi wa…
Ewe Mtakatifu Yuda Tadei,/ mtume mtukufu na shahidi wa Kristo,/ umesifika pote kwa wepesi wako wa kutoa misaada/ kwa wanaokukimbilia katika matatizo y…
Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina.SALA YA KUSHUKURUTunakushukuru, ee Mungu, kwa mapaji uliyotujalia leo. Amina.Baba yetu …Salam…
Enyi Yesu na Maria na Yosefu,nawatolea Moyo, na roho, na uzima wangu.Enyi Yesu na Maria na Yosefu,mnipokee saa ya kufa kwangu.Enyi Yesu na Maria na Yo…
Ee Yesu Mfungwa wa Upendo wa Mungu,/ ninapofikiri Upendo wako na jinsi ulivyojitolea kwa ajili yangu,/ nashindwa kuelewa./ Unaficha Ukuu wako usiofaha…
Discussion
Comments are public to read. Sign in to participate in the discussion.
You can read the discussion, but only logged-in AckySHINE users can post comments or replies.
Log in to participate