Sala ya Asubuhi ya kila siku

✍️ DIN - Melkisedeck Leon ShineπŸ“… 2016-01-17 08:58:00πŸ’¬ 83 comments⏱️ ~4 min read
πŸ“„ PDF
Kwa jina la Baba….. Ee Baba yetu Mungu mkuu,umenilinda usiku huu. Nakushukuru kwa moyo, ee Baba,Mwana na Roho. Nilinde tena siku hii,niache dhambi nikutii.Naomba sana Baba wee, baraka yako nipokee. Bikira safi, Ee Maria nisipotee nisimamie. Mlinzi mkuu malaika wee kwa Mungu wetu niombee,nitake nitende mema tu na mwisho nije kwako juu.Amina.

NIA NJEMA.

Kumueshimu Mungu wangu,namtolea roho yangu. Nifanye kazi nipumzike ,amri zake tu nishike. Wazo,neno,tendo lote namtolea Mungu pote Roho,Mwili chote changu. Pendo na uzima wangu. Mungu wangu nitampenda wala dhambi sitatenda. Jina lako nasifia,utakalo hutimia kwa utii navumili. Teso na matata pia,nipe Bwana neema zako, niongeze sifa yako.Amina.

SALA YA MATOLEO.

Ee Yesu kwa mikono ya Bikira Maria,na kwa maungano na sadaka yako kuu. Ninakutolea sala,matendo,masumbuko na furaha zangu zote za leo. Ee Yesu ufalme wako utufikie.Amina.

BABA YETU.

Baba yetu uliye mbinguni,jina lako litukuzwe. Ufalme wako ufike.Utakalo lifanyike duniani kama mbinguni. Utupe leo mkate wetu wa kila siku.Utusamehe makosa yetu,kama tunavyo wasamehe na sisi waliyo tukosea. Usitutie katika kishawishi,lakini utuopoe maovuni.Amina.

SALAMU MARIA.

Salamu Maria,umejaa neema Bwana yu nawe,umebarikiwa kuliko wanawake wote,na Yesu mzao wa tumbo lako amebarikiwa. Maria mtakatifu Mama wa Mungu,utuombee sisi wakosefu sasa na saa ya kufa kwetu.Amina.

KANUNI YA IMANI.

Nasadiki kwa Mungu,Baba Mwenyezi,muumba mbingu na dunia. Na kwa Yesu Kristu Mwanaye wa pekee,Bwana wetu aliyetungwa kwa Roho Mtakatifu,akazaliwa na Bikira Maria,akateswa kwa mamlaka ya ponsyo Pilato,akasulibiwa, akafa,akazikwa,akashukia kuzimu siku ya tatu akafufuka katika wafu, akapaa mbinguni amekaa kuume kwa Mungu Baba Mwenyezi,toka huko atakuja kuwahukumu wazima na wafu. Nasadiki kwa Roho Mtakatifu,kanisa takatifu katoliki ushirika wa Watakatifu,maondoleo ya dhambi,ufufuko wa miili na uzima wa milele.Amina.

AMRI ZA MUNGU.

1.Ndimi Bwana Mungu wako,usiabudu miungu wengine. 2.Usilitaje bure jina la Mungu wako. 3.Shika kitakatifu siku ya Mungu. 4.Waheshimu Baba na Mama upate miaka mingi na heri duniani. 5.Usiue. 6.Usizini. 7.Usiibe. 8.Usiseme uwongo. 9.Usitamani mwanamke asiye mke wako. 10.Usitamani mali ya mtu mwingine.

AMRI ZA KANISA.

1.Hudhuria misa takatifu domonica na sikukuu zilizo amuliwa. 2.Funga siku ya jumatano ya majivu,usile nyama siku ya Ijumaa kuuu. 3.Ungama dhambi zako walau mara moja kwa mwaka. 4.Pokea Ekarist takatifu hasa wakati wa Pasaka 5.Saidia kanisa katoliki kwa zaka. 6.Shika sheria katoliki za ndoa.

SALA YA IMANI.

Mungu wangu,nasadiki maneno yote linayo sadiki na kufundisha kanisa katoliki la Roma kwani ndiwe uliye fumbuliwa hayo,wala hudanganyiki na wala hudanganyi.Amina.

SALA YA MATUMAINI.

Mungu wangu,natumaini kwako nitapewa kwa njia ya Yesu Kristu,neema zako duniani na utukufu mbinguni.Kwani ndiwe uliyeagana hayo nasi nawe mwamini.Amina.

SALA YA MAPENDO.

Mungu wangu,nakupenda zaidi ya chochote, kwani ndiwe mwema ndiwe mwenye kupendeza. Nampenda na jirani yangu kama nafisi yangu kwa ajiri yako.Amina.

SALA YA KUTUBU.

Mungu wangu,nimetubu sana dhambi zangu kwani ndiwe mwema,ndiwe mwenye kupendeza wachukizwa na dhambi. Basi sitaki kukosa tena nitafanya kitubio,naomba neema yako nipate kurudi.Amina.

SALA KWA MALAIKA MLINZI.

Malaika mlinzi wangu,unilinde katika hatari zote za Roho na za Mwili.Amina.

MALAIKA WA BWANA.

K.Malaika wa Bwana alimpasha habari Maria. W.Naye akapata mimba kwa Roho mtakatifu. Salamu Maria….. K.Ndimi mtumishi wa Bwana. W.Nitendewe ulivyo nena. Salamu Maria….. K. Neno la Mungu akatwaa Mwili. W. Akakaa kwetu. Salamu Maria…. K. Utuombee Mzazi Mtakatifu wa Mungu. W. Tujaliwe ahadi za Kristu. Tuombe. Tunakuomba Ee Bwana utie neema yako mioyoni mwetu ili sisi tuliyojuwa kwa maelezo ya malaika kwamba, Kristu mwanao amejifanya mtu kwa mateso na msalaba wake. Tufikishwe kwenye utukufu wa ufufuko. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristu Bwana wetu.Amina.

ATUKUZWE BABA.

Atukuzwe Baba na Mwana na Roho Mtakatifu,kama mwanzo na sasa na siku zote na milele.Amina. K. Moyo Mtakatifu wa Yesu W.Utuhurumie. K. Moyo safi wa Bikira Maria. W. Utuombee. K. Mtakatifu Yosefu. W. Utuombee. K. Watakatifu somo wa majina yetu. W. Mtuombee. K.Watakatifu wote wa Mungu. W.Mtuombee. Kwa jina la Baba…..
πŸ’¬

Discussion

Comments are public to read. Sign in to participate in the discussion.

83 comment(s)
πŸ” Login required to comment or reply

You can read the discussion, but only logged-in AckySHINE users can post comments or replies.

Log in to participate
B
Betty Akinyi2022-02-08 14:37:49
Hauko peke yako; Mungu yuko nawe
R
Ruth Wanjiku2022-01-26 00:55:56
Kuna tumaini kwa ajili ya siku zijazo, maana Mungu anajua mipango aliyokupangia
E
Elizabeth Malima2021-12-18 05:27:32
Anaponya mioyo iliyovunjika na kufunga majeraha yao
C
Charles Mboje2021-11-23 22:12:19
Baraka kwako na familia yako.
R
Richard Mulwa2021-10-11 06:53:51
Katika udhaifu wetu, rehema za Mungu zinatupa nguvu
N
Nancy Komba2021-10-10 16:25:49
πŸ™πŸ’–πŸ™ Mungu akufunike na upendo
J
Jackson Makori2021-08-30 20:24:31
πŸ™πŸŒŸ Namuomba Mungu akupiganie
C
Catherine Mkumbo2021-04-21 13:20:59
Rehema hushinda hukumu
J
Janet Sumari2021-01-16 14:35:44
πŸ™β€οΈ Mungu ni mkombozi
V
Victor Kamau2021-01-13 11:53:57
πŸ™πŸ’–βœ¨ Neema yako ni ya kutosha
N
Nora Lowassa2020-12-27 17:16:13
Katika uwepo wake, kuna ukamilifu wa furaha
R
Ruth Wanjiku2020-12-21 22:49:53
Rehema zake ni ukumbusho wa daima wa upendo wake
P
Patrick Kidata2020-10-21 04:09:33
πŸ™β€οΈπŸ’– Baraka za Mungu ziwe nawe
J
John Mushi2020-08-26 20:15:45
Mungu ni mwaminifu; hatakuacha kamwe wala hatakupungukia
L
Linda Karimi2020-08-11 07:18:11
Kwa Mungu, yote yanawezekana
S
Samuel Were2020-05-04 22:19:02
Upendo wa Mungu na rehema zake havikosei kamwe
N
Nora Lowassa2020-04-18 14:20:51
Rehema za Mungu ni kubwa kuliko kosa lolote
J
Janet Sumari2020-01-13 18:03:58
Rehema za Mungu ni mpya kila asubuhi
D
Daniel Obura2020-01-13 06:52:09
πŸ™β€οΈ Mungu akubariki
V
Victor Kamau2020-01-11 21:47:23
πŸ™β€οΈπŸŒŸ Asante Mungu kwa uhai