SALA YA KUANGUKA MIGUUNI PA BWANA YESU KATIKA EKARISTI

✍️ DIN - Melkisedeck Leon ShineπŸ“… 2017-10-01 15:40:00πŸ’¬ 83 comments⏱️ ~2 min read
πŸ“„ PDF

Ee Yesu Mfungwa wa Upendo wa Mungu,/ ninapofikiri Upendo wako na jinsi ulivyojitolea kwa ajili yangu,/ nashindwa kuelewa./ Unaficha Ukuu wako usiofahamika/ na kujidhihirisha kwa ajili yangu mimi mnyonge./ Ee Mfalme wa utukufu,/ unaficha uzuri wako,/ lakini jicho la moyo wangu/ linapenya pazia na kuona Majeshi ya Malaika/ wakikuimbia kwa heshima bila kukoma/ na nguvu zote mbinguni zikikusifu bila mwisho zikisema:/ β€œMtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu..”/

Ni nani awezaye kufahamu Upendo wako/ na huruma yako isiyo na kipimo kwa ajili yetu!/ Ee Mfungwa wa Upendo,/ nafungia moyo wangu masikini/ kwenye Tabarnakulo hii/ ili niweze kukuabudu usiku na mchana bila mwisho./ Najua hakuna kizuizi/ na hata kama naonekana kukaa mbali,/ lakini moyo wangu u pamoja nawe/ katika ibada hii./ Hakuna kinachoweza kuzuia upendo wangu kwako./ Kwangu hakuna kizuizi chochote./

Ee Utatu Mtakatifu,/ Mungu Mmoja usiyegawanyika,/ utukuzwe kwa zawadi yako hii kuu/ na agano hili la huruma!/

Nakuabudu,/ Bwana na Muumba uliyefichika katika Sakramenti Takatifu!/ Ee Bwana,/ nakuabudu kwa kazi zote za mikono yako/ zinazonifunulia Hekima yako kuu,/ Wema wako na Huruma yako kuu./ Uzuri uliousambaza hapa/ Uzuri ulio nao Wewe mwenyewe/ ambaye U Uzuri usioelezeka;/ na ingawaje umejificha na kusitiri uzuri wako,/ jicho langu,/ kwa mwanga wa imani linafika kwako,/ na roho yangu inapata kumtambua Muumba wake/ aliye Uzuri usiopimika,/ ulio juu ya kila uzuri,/ na moyo wangu unazama kabisa katika sala ya kukuabudu./

Bwana wangu na Muumba wangu,/ wema wako wanitia moyo wa kuongea nawe,/ Huruma yako huondoa kiambaza/ kitenganishacho Muumba na kiumbe./ Furaha ya moyo wangu,/ ee Mungu, ni kuongea na Wewe./ Yote ambayo moyo wangu unayatamni nayapata kwako./ Hapa ndipo mwanga wako unaponiangaza akili yangu/ na kuiwezesha kukujua Wewe zaidi na zaidi/ – ndipo mikondo ya neema inapoutiririkia moyo wangu,/ ndipo roho yangu inapochota uzima wa milele./ Ee Bwana na Muumba wangu,/ licha ya mapaji yote haya,/ unajitoa mwenyewe kwangu,/ ili uweze kujiunganisha na kiumbe dhaifu na maskini./

Ee Kristu,/ nafurahi sana nionapo kwamba unapendwa/ na kwamba sifa na utukufu wako vinaongezwa/ hasa ya Huruma yako./ Ee Kristu,/ sitaacha kamwe kuutukuza wema wako na huruma yako,/ hadi dakika ya mwisho ya maisha yangu./ Kwa kila tone la damu yangu/ na kwa kila pigo la moyo wangu/ naitukuza Huruma yako./ Natamani kugeuzwa kabisa/ na kuwa utenzi wa utukufu wako./ Naomba siku ya kufa kwangu/ popote nitakapokuwa nimelala,/ pigo la mwisho la moyo wangu/ liwe utenzi mpendevu/ usifuo Huruma yako isiyo na kipimo./ Amina

(Na Mt. Faustina Kowalska).

πŸ’¬

Discussion

Comments are public to read. Sign in to participate in the discussion.

83 comment(s)
πŸ” Login required to comment or reply

You can read the discussion, but only logged-in AckySHINE users can post comments or replies.

Log in to participate
J
John Mwangi2024-06-10 19:24:10
πŸ™β€οΈπŸ’– Bwana akujalie baraka
P
Peter Tibaijuka2024-04-13 05:01:22
Imani ni kuwa na uhakika wa kile tunachotarajia na kujua kwa hakika kile ambacho hatuoni
R
Robert Okello2024-03-17 06:36:23
Bwana atapigana kwa ajili yako; wewe unahitaji tu kutulia
S
Samson Mahiga2024-02-12 10:23:40
Baraka kwako na familia yako.
S
Stephen Kikwete2024-01-23 08:13:45
πŸ™β€οΈ Mungu akubariki
A
Alice Mwikali2023-12-28 17:14:37
Hadithi yako haijaisha; Mungu bado anaandika
B
Bernard Oduor2023-09-13 04:44:19
Mwamini Bwana; anajua njia
C
Christopher Oloo2023-09-09 10:48:38
πŸ™β€οΈβœ¨ Mungu akujalie furaha
M
Margaret Mahiga2023-08-12 04:21:07
Wacha imani yako iwe kubwa kuliko hofu yako
N
Nancy Akumu2023-04-29 11:46:28
Rehema hushinda hukumu
R
Rose Lowassa2023-03-03 00:10:22
Tumaini ni nanga ya roho
N
Nora Kidata2023-02-09 11:58:59
Dumu katika Bwana.
E
Edward Chepkoech2023-01-17 23:43:19
Imani inaweza kusogeza milima
C
Christopher Oloo2023-01-06 13:06:51
Wakati wa Mungu ni kamilifu
A
Ann Awino2022-12-11 14:48:23
Neema na amani iwe nawe.
C
Catherine Mkumbo2022-11-14 15:23:59
Rehema za Mungu ni kubwa kuliko kosa lolote
C
Chris Okello2022-10-20 21:39:37
Anaponya mioyo iliyovunjika na kufunga majeraha yao
M
Mariam Hassan2022-10-14 18:17:15
Mungu ni kimbilio letu na nguvu zetu, siku zote tayari kusaidia wakati wa shida
A
Alex Nakitare2022-07-28 16:05:00
πŸ™βœ¨ Mungu atakuinua
L
Lucy Mushi2022-07-14 13:43:56
πŸ™πŸ’– Nakusihi Mungu