
Kushindwa jambo sio Makosa
Kushindwa jambo sio Makosa, bali kuacha kufanya jambo kabisa ni makosa makubwa.
Browse published Articles by category, tag or language. Random discovery is the default and keeps a stable order while you move through pages.

Kushindwa jambo sio Makosa, bali kuacha kufanya jambo kabisa ni makosa makubwa.

Hakuna uwezo bila fursa. Huwezi kusema unauwezo wa kitu kama hauna fursa ya kukifanya.

Biashara ya maisha ni kusonga mbele tuu. Maisha hayarudi nyuma wala hayafai kurudisha nyuma. Maisha yanasonga mbele.

Tofauti ya maskini, tajiri na mwenye uchu/tamaa ni kwamba; Mtu maskini anafanyakazi ili apate chochote, tajiri anafanya kazi apate vitu vingi lakini mwenye uchuβ¦

Maisha ya ujana ni kufanya mema au mabaya, kushinda au kushindwa. Uzee ni sherehe au majuto ya ujana.

Huwezi kupata maendeleo kwa kusitasita na kuogopaogopa. Hata kobe anayesonga mbele ni yule anayetoa kichwa chake kwenye gamba/nyumba yake.

Uwe mzuri kwenye kufanya kama ulivyo kwenye kufikiri. Matendo yako yafanane na maneno na maneno na matendo.


Tamaa ni tabia ya kiasili ya kila mtu, tofauti ya mtu na mtu ni namna ya kukabili tamaa.

Kwenye dunia hii vitu haviwezi kusimama kama havijasimamishwa.

Ukiweza kutumia vizuri kipaji au uwezo mdogo ulionao itakufanya uwe bora na mwenye sifa nzuri kuliko yule mwenye uwezo mkubwa.

Tunatakiwa tujenge uhodari na uwezo utakaotusaidia kutumia fursa zilizo wazi mbele yetu.

Ukitaka kufanya biashara kwa ufanisi; wakati wa kununua nunua ukiwa na mtazamo wa muuzaji kwa kufikiri kama wewe ungekua ndio unauza ungeuzaje, na Wakati wa kuuβ¦

Tunatakiwa tujithaminishe wenyewe kwa yale tunayoona tunauwezo wa kuyafanya japokuwa watu wengine wanatuthamanisha kwa yale wanayoyaona tumeshayafanya

Vile unavyotoa ndivyo unavyopokea. Yule anayetoa sana ndiye ansyepokea sana. Kutoa ni kuhifadhi.

Kitu chochote kinapofanywa vizuri mwanzoni ni sawa na kimefanywa nusu tayari.

Jarbu Mambo mengi kadiri uwezavyo kwani kwa kujaribu ndivyo tunajua tunaweza au hatuwezi. Kamwe usiseme huwezi jambo kabla ya kujaribu.

Ukiona unaweza ukakaa siku nzima bila hata kuwa na wazo moja jipya ujue umezeeka akili tayari na kesho unaweza ukawa haupo

Usimpe mtu ushauri ambao unahisi ataukubali sana, mpe mtu ushauri wenye manufaa kwake japo ni mgumu kuukubali.

Uwezo wa kuwa makini katika jambo bila kuyumbishwa na kitu chochote ni ishara kuu ya mtu mwenye akili na mwenye mafanikio.

Kujaribu kufanya jambo kubwa la kipekee ni kushinda hata kama halijafanikiwa.

Changamoto na ugumu wa jambo upo kwa wale wanaolifanya. Huwezi kukaa na kutazama jambo bila kulifanya na kisha kujua changamoto zake.

Katika maisha, kinga kuu ya magonjwa na majanga yote ni kujikatalia au kujinyima.

Huwezi kuona thamani ya kitu ambacho hujakigharamia. Faida haina thamani kama haijagharamiwa.