Log in to access your menu with tools for managing π tasks, π₯ clients, π° finances, π learning, π personal growth, and π spirituality, all in one place!.
Welcome to AckySHINE, your go-to platform for personal growth, productivity, and well-being, offering tools tailored to organize your life, manage finances, and deepen your journey.
Angalia pombe ilichomfanya huyu jamaa, kweli pombe haimuachi mtu salama
Updated at: 2024-05-25 16:56:22 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Leo nimeiogopa pombe.
Nimetokea kuiogopa pombe baada ya kumwona jirani yangu akicheza muziki kwa sauti ya jenereta langu, akidhani yuko clubβ¦..nkamsikia anasema "wee dj noomaaaa"
Baada ya kuzima jenereta akaniuliza uo mziki kaimba nan?
Nlivyokuwa na roho mbaya Nikamwambia iyo ni collabo ya Yamaha na Petrol πππππ
Updated at: 2024-05-25 17:03:30 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Bosi wangu karudi safari yake kutoka serengeti..! Si akanitumia picha, lakini ilikuwa network yenyewe tabu.. kwahio picha haikufunguka na kwa vile niliona itachelewa kufunguka na ataona sikumjibu basi nami..
Nikampelekea msg nikamuandikia umependeza saana bosi mashaallahβ¦!! sasa baada tu ya kumfika msg.. na huku picha ikafunguka kumbe picha ya Sokwe..!! Basi Kaniambia kesho niende ofsini kwake kuna barua yangu.. Nahisi hyo barua ina pesa, hapa cjalala, nmekosa usingizi kabisa,nawaza ninunulie nn hyo pesa.Na kesho asubuhi sa 12 asubuhi atanikuta ofisini kwake naisubiri barua, sipendagi ujinga mimi.
Updated at: 2024-05-25 17:13:37 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mama alichukuwa simu akampa mwanawe. Mama..Mpigie babako mwambie chakula tayari. (Mtoto akachukuwa na kupiga) Mtotoβ¦Mama simu ya baba imepokelewa na mwanamke. (Mama kwa hasira) Akirud atanitambua leo. (Baada ya muda kidogo baba akarud,kufika mlangon tu kapokewa na sufuria ya kichwa. Hajakaa vzur mwiko wa pua) Mama..Mwanangu ulipopiga simu ya babako mwanamke wake alisemaje?? Mtoto..Alisema mteja unaempigia hapatikan kwa sasaβ¦..
Alichokifanya jamaa baada ya kuokota wallet yenye pesa za kumwaga
Jamaa aliokota wallet, alipofika nyumbani akapiga simu kwenye radio station
"Naitwa John nimepiga simu kutangaza kuwa nimeokota wallet ndani ina laki 7, ATM Card na kikaratasi chenye PIN ya ATM Card na kijimkufu cha dhahabu kinene hiviβ¦"
Updated at: 2024-05-25 18:04:09 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Jamaa aliokota wallet, alipofika nyumbani akapiga simu kwenye radio station
"Naitwa John nimepiga simu kutangaza kuwa nimeokota wallet ndani ina laki 7, ATM Card na kikaratasi chenye PIN ya ATM Card na kijimkufu cha dhahabu kinene hiviβ¦"
Mtangazaji akasema:- Akhasante sana John, kwa hiyo ungependa kumrudishia mwenyewe kama ana kusikiliza akutafute kwa No. Gani!?
John: Hapana, mi nilikuwa namshukuru tu maana amenitoa kwenye matatizo na ninapenda kumuombea Dedication wimbo wa Snura "MAJANGA" umfikie popote pale alipoβ¦!!!
Dereva alikamatwa kwa kosa la kusababisha ajari ya watu wa5 aliowagonga. Trafik akamuliza kwanin umewagonga awa watu? Jamaa akajibu,"nilikua mwendo wa kasi sana, alafu nimejaza abiria ndani, gari likawa linakuja mbele yangu nilipokanyaga breki zikakatika, sasa ningefanya nin?"
Updated at: 2024-05-25 18:03:22 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Dereva alikamatwa kwa kosa la kusababisha ajari ya watu wa5 aliowagonga. Trafik akamuliza kwanin umewagonga awa watu? Jamaa akajibu,"nilikua mwendo wa kasi sana, alafu nimejaza abiria ndani, gari likawa linakuja mbele yangu nilipokanyaga breki zikakatika, sasa ningefanya nin?" Trafki akamwmbia, kwanin ucngeenda upande ambao una watu wachache ili uokoe wengi? Jamaa akajibu, "nilifanya hivo, huku kushoto alikua m1 na kulia walkua wa4, nikamfuata uyu wa kushoto et akakambilia upande wakulia akazani cjamwona, nikamfata huko huko alipoenda, nikampa kitu mbwa yule"
Updated at: 2024-05-25 17:59:16 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Huwa naenjoy sana kusoma yaliyoandikwa nyuma ya daladala hasa ninapokuwa kwenye foleni. Misemo maarufu ya kwenye daladala.
1.Yatima hadeki 2.Utamu wa chips mimba 3.Ukitaka kujua ugumu wa kudai kopesha ukweni 4. Usiyempenda kaja 5. Kobe hapimwi joto 6. Acha kazi uone kaz kupata kaz 7. Ukichezea koki utalowa 8. Heshima pesa kipara kovu tu! 9. Mtumbwi hauna saitmira. 9. Silaha pesa bastola mzigo 10. Hata uoge mjini huendi 11. Chezea mshahara usichezee kazi. 12. Ukiona manyoya ujue kishaliwa 13. Ikisimama Panda 14. Pombe pombe tuu kunywea bar mbwebwe 15. Njia ya chooni haioti nyasi 16. Likizo ya maskini ugonjwa 17. When i grow up i want to be a scania 18. Hata bibi alikuwa binti 19. Kisigino hakikai mbele 20. Kama mapenz pesa kaolewe na benki 21. Hata barabara ina matuta lakin huwez panda viazi 22. Mavi hayana miba lakin ukikanyaga lazma uchechemee 23. Paka haishi kwa msela 24. Ukipendwa ujue kuna boya kaachwa 25. NIPO NIPO KWANZA 26. Mchana nzi ucku mbu 27. Ucmshangae funza kukata viuno ndio mwendo wake 28. Kama umelipenda(gari) bonyeza nyota liwe lako 29. Supermarket hawauzi mkaa 30. We nisubiri mi nakungoja. 31. Zetu dagaa kuku tamaa 32. Hata uwe na heshima vipi huwezi kumpokea askari bunduki H ππππππππππ
Updated at: 2024-05-25 17:52:36 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
_Sheria inasema kila anaetembea na chombo cha moto barabarani sharti awe na leseni._ _Sasa hawa wauza kahawa mbona wanatembea na chombo cha moto lakini hawakamatwi π‘._ _Hizi sheria zinapendelea._ πππππππππππ