Log in to access your menu with tools for managing 📝 tasks, 👥 clients, 💰 finances, 📖 learning, 🔍 personal growth, and 🌟 spirituality, all in one place!.
Welcome to AckySHINE, your go-to platform for personal growth, productivity, and well-being, offering tools tailored to organize your life, manage finances, and deepen your journey.
Updated at: 2023-04-29 22:52:35 (3 years ago by Melkisedeck Leon Shine)
Baba- : Halloo mke wangu.. yaani ni shida sitaweza kurudi nyumban, daraja limevunjika na kutoka morogoro kurudi dar haiwezekani MAMA:- Mme wangu morogoro ulienda bila kuniaga! ? BABA:- Ilikuwa ni ghafla sana mke wangu sikuweza kukwambia MAMA:- kha! Sasa watoto nani atawaangalia BABA:- Unasemaje! We uko wapi kwan MAMA:- Niko bagamoyo na daraja limeondolewa na maji sitaweza kurudi. BABA:- Unasemaje we mwanamke.. nakwambia nikukute nyumban ndani ya dk 15 Baada ya dk 15 Baba kafika nyumban. MAMA:- Haya umefkaje kutoka morogoro? BABA:- Nimepewa lift na helkopta ya Mbowe..
Updated at: 2024-05-25 17:04:59 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Nimefika hapa Polisi Station nimefarijika sana na Kustuka baada ya kumkuta Askari hapa Kaunta anasoma Biblia nikajisikia fahari kuona anasoma neno kituo cha Polisi. Nikamuukiza Afande ni Nani alimuua Goliathi? Akasema Muulize Afande Mwita mlango namba 2 ndo anausika na Kesi za Mauaji.😂😂
Updated at: 2024-05-25 17:46:44 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Baba na mama baada ya kurudi safari pamoja wakakuta BARUA iko mezani SEBULENI ikisema…. "Baba na mama, ni matumaini yangu kuwa mtasoma ujumbe wangu huu kwenye karatasi niliyoiweka juu ya meza, naomba msishtuke mana ni mambo ya kawaida kwenye maisha tunayoishi, najua mtaumia kwa vile bado nasoma na ndiyo nipo kidato cha kwanza…" Napenda kuwajulisha kwamba sasa hivi mnaposoma hii barua sipo nyumbani, nimetoroka mana nimegundua nina uwezo wa kujitegemea kwa sababu mi ni kijana mwenye umri wa miaka 14 na ninajua kipi chema na kipi kibaya.
Tangu mwezi mmoja uliopita nilikuwa na uhusiano nabinti mmoja aliyeitwa Rachel, mwenye umri wa miaka 27 na kwa sasa ndo naishi naye kwenye chumba alichopanga. Nilipokuwa nyumbani sikuwa napata hela za kutosha ila sasa nimeanza kushika noti za shilingi 10,000… Msichana niliyenaye ni mzuri sana wa umbo na ninampenda sana, amenifundisha njia za kutafuta hela.
Amenipangia kazi ya kuuza madawa ya kulevya na yeye ikifika usiku anaenda kuuza mwili wake, basi kila siku tunapata hela ya kutosha, huyu mchumba wangu ni msichana mwenye bidii, kwa siku analala masaa 6 tu maana mwanaume yeyote akija lazima awe naye chumbani kwa muda wa masaa 3.
Msiwe na hofu, nipo salama kabisa na nimeamua kumwoa Rachel mana ni kila kitu kwangu. Pia amenunua gari la kubebea mbao kwahiyo biashara inaenda vizuri.
Rachel ameenda kupima afya na amekutwa na upungufu wa kinga mwilini, mara nyingi namridhisha anapotaka kitu flani, iwe kufanya naye mazoezi ya viungo au kufanya naye mapenzi, si mnajua unapokuwa na mgonjwa unakuwa naye karibu.
Ila mi pia sijihisi vizuri mana kila saa nakohoa tu na sina uhakika kama nimeathirika. Tumepanga baada ya miaka miwili tutawatembelea, nadhani mpaka miaka miwili iishe atakuwa ameshajifungua, na ni furaha yangu mtamwona mjukuu wenu. Wazazi wangU, sina la kuongeza kwaherini Mungu akipenda tutaonana.
NB: "Baba na mama, mimi nipo chumbani kwangu najisomea, mnachokisoma ni h/work ya mwalimu wa kiswahili alituambia tutunge hadithi fupi ya kusisimua, naomba muiangalie kama kuna makosa!"
Ingekuwa wewe hapo ndi baba au mama ungefanyaje? SHARE na wenzako wasome.
Padri Akimbia wakati wa kuungamisha, chanzo ni hiki
Padri alikuwa amekaa katika confession booth kanisani
peke yake.
Mara kukaingia jamaa mmoja akapiga magoti upande wa
pili, akafanya ishara ya msalaba kisha akaanza kuungama
{confess}
"Padri nimekuja kuungama dhambi zangu, leo nimefanya
dhambi kubwa sana."
Padri, "Endelea…"
Updated at: 2023-04-29 22:53:14 (3 years ago by Melkisedeck Leon Shine)
Padri alikuwa amekaa katika confession booth kanisani peke yake. Mara kukaingia jamaa mmoja akapiga magoti upande wa pili, akafanya ishara ya msalaba kisha akaanza kuungama {confess} "Padri nimekuja kuungama dhambi zangu, leo nimefanya dhambi kubwa sana." Padri, "Endelea…"
"Bosi wangu aliniita nyumbani kwake, akaniambia amegundua nimeiba shilingi millioni 100 kazini. Akasema nisipozitoa atanipeleka polisi, sa kwa ukweli mi naogopa kufungwa. Nikatazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke yetu,nikatoa bastola nikamuua….. Yesu atanisamehe?"
Padri: "Utasamehewa." "Basi wakati nataka kuondoka nikasikia mlango unafunguliwa kutazama, Loh! Mke wa bosi, alipoona kilichotokea akasema anapiga polisi simu. Kutazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke yetu, nikamuua na yeye pia… Yesu atanisamehe hilo?" Padri: "Utasamehewa."
Nikatoka nje, nikawasha gari niondoke, lakini mlinzi akakataa kunifungulia, ati amesikia mlio wa bastola. Nikaona ataniletea kizuizi huyu. Nikatazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke yetu, nikamuua….. Yesu atanisamehe?" Padri:"Utasamehewa."
"Nikajifungulia geti mwenyewe nikaenda nyumbani, wakati napanga kuja kuungama mtoto wa bosi akabisha hodi, nikawaza mambo gani tena, akasema alirudi nyumbani na kukuta yaliyotokea akanionesha diary ya babake, inayoonesha nilikuwa na appointment naye wakati nilipomuua. Nikamuuliza nani mwingine anayejua? Akasema ameanzia kwangu kisha anaenda polisi.
Nikatazama huku na huku nikakuta tuko wawili peke yetu, nikamuua….. Yesu atanisamehe na hilo?"
Kimyaa…. "Padri yesu atanisamehe?" kimya….
Jamaa akatazama kwenye confession booth padri hayupo, lakini kwenye kona moja akaona kabati la nguo za mapadri linatikisika. Kufungua akaona padri kajificha ndani anatetemeka huku akitokwa na jasho.
Jamaa, "Sasa baba mbona umekimbia?" Padri kwa taabu akajibu, "Nilitazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke yetu……."
Updated at: 2024-05-25 18:00:42 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Jamaa fulani alikuwa ame2lia beach mzungu akapita akamuliza "Are u relax ? Jamaa akawa hamuelewi akamjibu No! Mzungu mwengine akapita akamuliza vilevile akajibu No!
Akaona hapa anasumbuliwa akasogea mbele kidogo ya maji akamuona mzungu mmoja alikuwa ame2lia. Akamuliza "are u relax? Mzungu akajibu yes jamaa akamkata makofi mawili na kumwambia kumbe we ndo relax inuka unatafutwa na wenzako…..Shenz mkubwa mie nasumbuliwa na wenzako kule we umejikausha!!
Updated at: 2024-05-25 17:18:04 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Looku Looku* 👀👀
*Ama Kweli Mkuki Kwa Nguruwe kwa Binadamu Mchungu Skia Hii….!!*
*Ishawahi kutokea Pale nilipokutana njiani na mwalimu aliyekufundisha MATHS secondary afu akaniambia nimuelekeze njia ya kwenda sehemu fulani.*
*_Nenda mbele kama 2KM hivi kisha kata kushoto,ila hakikisha ANGLE inakuwa ni 30.5 KUSINI MASHARIKI.Kisha tumia PYTHAGORAS na hakikisha una FOUR FIGURE ili kupata thamani ya ANGLE._*
*Mwalimu alisonya na kuondoka.*😏😏😏😒😒
*Stakagi ujinga kabisa mimi, wakati ananichapa alifikiri sifa*😂😂
😅🙌🏽🙌🏽 *Mniache Tuu Mimi Sio Kwa Bifu Ilo Aiseee*🏃🏾
Updated at: 2024-05-25 17:09:40 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mtoto wa miaka sita alimuuliza babake: MTOTO: Baa, eti sisi wanadamu tulikuja vipi duniani? BABA: Mungu alimuumba Nabii Adam na Hawa. Kisha wao wakaanza kuzaa watoto na watoto wakazaa mpaka tukazaliwa sisi. (Mtoto hakuridhika akamfuta mamake) MTOTO: Mma, eti sisi wanadamu tulikuja vipi duniani? MAMA: Wanasayansi wamesema sisi tulitokana na manyani baadae tukawa binadamu. (Mtoto akarudi kwa baba) MTOTO: Baa mbona mama ansema sisi tulikuwa manyani mwanzo?Au wanidanganya? BABA: Mwanangu, mimi nimekuelezea kuhusu ukoo wetu. Mamako amekuelezea kuhusu ukoo wao😂😂🚶🏼🚶🏼🚶🏼