ACKYSHINE ARTICLE Β· PRINTABLE READER

Zifahamu dhambi ambazo huondolewa na PAPA pekee au Padre kwa ruhusa maalumu kutoka kwa Baba Mtakatifu

✍️ DIN - Melkisedeck Leon ShineπŸ“… December 2, 2020πŸ’¬ 50 comments
πŸ—‚οΈ Mafundisho ya Msingi ya Kanisa Katoliki: Makala za Katoliki#Karibu AckySHINE#Katoliki: Baba Mtakatifu#Katoliki: Imani ya Kanisa Katoliki#Katoliki: Kutubu na Kusamehewa dhambi#Katoliki: Sakramenti ya Kitubio🌐 Kiswahili
Zifahamu dhambi ambazo huondolewa na PAPA pekee au Padre kwa ruhusa maalumu kutoka kwa Baba Mtakatifu
1.Kumdhuru baba mtakatifu kimwili mfano:kumpiga au kumtemea mate
2.Kukufuru Ekaristi Takatifu mfano kutema na kuchezea kwa namna yoyote kama ya kishirikina.
3.Padri kutenda dhambi na muumini mfano : kuzini
4.Askofu kumpa padre uaskofu padre yeyote bila ruhusa ya baba mtakatifu.
NB:jiandae kufanya kitubio kama unaguswa na dhambi yoyote kati ya hizo kwani kuna mchakato maalumu wa kuteuliwa kwa mapadre zaidi ya 800 na baba mtakatifu kwenda dunia zima kwa kuwaondolea watu wenye dhambi hizo. Tumsifu Yesu Kristu πŸ™πŸΏ
Kuhusu dhambi namba 3 inakosa tu maelezo.Na maelezo yake ni haya;
Padre kuzini na muumini hiyo inabaki kuwa ni dhambi Kati ya Padre na muumini wake.Kwa dhambi hiyo Padre anaweza akatafuta Padre mwenzake akaungama kadhalika na kwa muumini huyo.
Shida ni pale tu endapo,Padre anataka KUMUUNGAMISHA mwanamke (muumini) aliyetoka KUZINI naye au yule ANAYEZINI naye hiyo dhambi na kosa hilo hata Askofu wako hana mamlaka ya kukuungamisha wala kukusamehe ni kiti cha Baba Mtakatifu pekee chini ya Congregatio inayoshughulikia mambo matakatifu iitwayo kwa kifupi CDF yaani Congregation for Doctrine of Faith.
Ambayo inashughulikia na mambo mawili hasa makuu yaani;
1.Protection of Sanctity of Sacraments
2.Dealing with Grave Disorders and bad conducts in the Church.
Kwa ufupi ndio hivyo ninaweza kukwambia.
βœ…
Direct PDF download

The download button now generates the PDF on the server. It no longer depends on an off-screen browser canvas, so the former blank-PDF capture path is bypassed.