SALA KWA MT. YOSEFU KUOMBA KUFAHAMU WITO WAKO
ποΈ Sala za Katoliki: Sala Muhimu Kwa Mkristu Mkatoliki#sala#Sala kwa Watakatifu#Sala za Maombi#Sala za Novenaπ Kiswahili

Ee uliye Mkuu, Mt. Yosefu, uliyatii kabisa maongozi ya Roho Mt. Unijalie neema ya kufahamu aina ya maisha ambayo Mungu anapenda mimi niishi. Usiniache nidanganyike katika jambo muhimu kama hili, ambalo furaha yangu hapa duniani inalitegemea, na hata pia wokovu wa roho yangu.
Unijalie, nikiangazwa na matakwa matakatifu na nikiwa mwaminifu katika kuyatimiza, nikumbatie aina ya maisha ambayo Mungu ameniandalia na yatakayoniongoza kwenye furaha ya milele.
Amina.
β
Direct PDF download
The download button now generates the PDF on the server. It no longer depends on an off-screen browser canvas, so the former blank-PDF capture path is bypassed.