ACKYSHINE ARTICLE Β· PRINTABLE READER

Sala ya Malaika wa Bwana

✍️ DIN - Melkisedeck Leon ShineπŸ“… January 17, 2016πŸ’¬ 83 comments
πŸ—‚οΈ Sala za Katoliki: Sala Muhimu Kwa Mkristu Mkatoliki#sala#Sala kwa Watakatifu#Sala za Kushukuru#Sala za Maombi🌐 Kiswahili
Sala ya Malaika wa Bwana

Malaika wa Bwana alimpasha habari Maria, naye akapata mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. Salamu Maria,….

Ndimi Mtumishi wa Bwana, nitendewe ulivyonena. Salamu Maria, ……
Neno wa Bwana akatwaa Mwili, akakaa kwetu. Salamu Maria, …..

Utuombee, ee Mzazi Mtakatifu wa Mungu, tujaliwe ahadi za Kristo.

Tuombe:

Tunakuomba ee Bwana, utie neema yako mioyoni mwetu, ili sisi tuliojua kwa maelezo ya Malaika, kwamba, Kristo Mwanao amejifanya mtu: kwa mateso na Msalaba wake, utufikishe kwenye utukufu wa ufufuko. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristo Bwana wetu, Amina.

βœ…
Direct PDF download

The download button now generates the PDF on the server. It no longer depends on an off-screen browser canvas, so the former blank-PDF capture path is bypassed.