ACKYSHINE ARTICLE Β· PRINTABLE READER

Ni vizuri kujua haya

✍️ SW - Melkisedeck ShineπŸ“… April 11, 2015πŸ’¬ 0 comments
πŸ—‚οΈ Biashara - Mbinu za Ujasiriamali na Biashara Kufanya tofauti#Karibu AckySHINE#SMS, Vichekesho, Mahusiano, Biashara na Ujasiriamali, Afya, Chemsha Bongo, Dini pamoja na Vitabu kwenye PDF#Ujasiriamali: Kujitambua na Kuwa na Mafanikio Katika Maisha#Ujasiriamali: Matumizi ya Fedha#Ujasiriamali: Mbinu za Kuwa Tajiri🌐 Kiswahili
Ni vizuri kujua haya

πŸ‘‰πŸΏDegree au vyeti ulivyo navyo haviwezi kukupa mafanikio.
πŸ‘‰πŸΏUzuri ulio nao hauwezi kukupeleka kwenye ndoto zako.
πŸ‘‰πŸΏUsipobadilisha hao marafiki ulio nao hutofika mahali popote.

πŸ‘‰πŸΏUsipobadilisha vitendo unavyovifanya kila siku hivyo hivyo mafanikio utayasikia kwa wengine.

πŸ‘‰πŸΏKazi au ajira unayoifanya usipojiongeza haiwezi kukupeleka kwenye maisha unayoyataka.

πŸ‘‰πŸΏHuo mshahara unaolipwa usipoutumia vizuri na kujiwekea akiba au kuwekeza kidogokidogo hutoacha kulalamika kila siku mshahara mdogo au hautoshi.

πŸ‘‰πŸΏUsipoacha kukopa bila malengo mafanikio ni ngumu kuyapata.

πŸ‘‰πŸΏUsipowekeza muda kwa ajili ya kujifunza na kuelewa mambo mengi ya biashara na ujasiriamali kwa ujumla na kufahamu dunia imetoka wapi,iko wapi na inaelekea wapi huytoacha kulalamika.

πŸ‘‰πŸΏUsipolipia gharama za kujifunza na ukajifunza kweli kile unachoelekezwa ikiwa ni pamoja na Pesa na muda haya mambo waachie wengine.

πŸ‘‰πŸΏUsipobadili fikra na mtazamo wako huwezi kubadilisha chochote katika maisha yako.

πŸ‘‰πŸΏUkiacha kusikiliza kila aina ya ushauri unaopewa na ndugu zako,jamaa zako,marafiki zako,familia yako,majirani zako na kujisikiliza wewe mwenyewe utahangaika sana.

πŸ‘‰πŸΏUsipofanya bidii na juhudi na ukakubaliana na changamoto zozote utakazokutana nazo maisha yatakuwa magumu sana kwako.

Kumbuka mtu pekee Wa kuyabadilisha maisha yako na kukusaidia kufikia malengo na ndoto zako wala sio mwingine ni mmoja tu nae ni WEWE.
Badilisha fikra zako,badilisha mtizamo wako,badilisha maisha yako.

βœ…
Direct PDF download

The download button now generates the PDF on the server. It no longer depends on an off-screen browser canvas, so the former blank-PDF capture path is bypassed.