ACKYSHINE ARTICLE ยท PRINTABLE READER

Ujumbe kwako wewe mwajiriwa au uliyejiari

โœ๏ธ SW - Melkisedeck Shine๐Ÿ“… January 10, 2015๐Ÿ’ฌ 0 comments
๐Ÿ—‚๏ธ Biashara - Mbinu za Ujasiriamali na Biashara Kufanya tofauti#Karibu AckySHINE#SMS, Vichekesho, Mahusiano, Biashara na Ujasiriamali, Afya, Chemsha Bongo, Dini pamoja na Vitabu kwenye PDF#Ujasiriamali: Matumizi ya Fedha#Ujasiriamali: Mbinu za Kuwa Tajiri๐ŸŒ Kiswahili
Ujumbe kwako wewe mwajiriwa au uliyejiari

Kama umeajiriwa au pia umejiajiri ni mojawapo ya njia zinazokuingizia kipato maana wengi wanaanzia hapo mpaka kuja kufikia kule wanakohitaji.
Ila kuna maswali machache ya kukupa changamoto ambayo nataka ujiulize:-

Kwako muajiriwa

๐Ÿ‘‰๐ŸฟUmeshawahi kujiuliza huo mshahara unaolipwa unakutosha kukutimizia Yale yote unayohitaji maishani mwako??

๐Ÿ‘‰๐ŸฟUmeshawahi kujiuliza ukifukuzwa au ukipunguzwa kazini utafanya nini?

๐Ÿ‘‰๐ŸฟUmeshawahi kujiuliza ofisi au kampuni unayofanyia ikifilisika wewe utafanya nini?

๐Ÿ‘‰๐ŸฟUmeshawahi kujiuliza kwa nini unataka kuhama au kuacha kazi hapo unapofanyia uende ofisi nyingine??

๐Ÿ‘‰๐ŸฟUmeshawahi kujiuliza kwanini hupapendi hapo unapoishi lakini bado unaendelea kuishi hapo?

๐Ÿ‘‰๐ŸฟUmeshawahi kujiuliza kwa nini huo usafiri unaoutumia huupendi lakini kila siku unautumia huo huo??

๐Ÿ‘‰๐ŸฟUmeshawahi kujiuliza ni kwa nini wanao au watoto wako hawapendi shule wanayosoma lakini wewe uwezo wako ndipo ulipoishia??

๐Ÿ‘‰๐ŸฟUmeshawahi kujiuliza kwa nini hupendi mikopo lakini bado unaendelea tu kukopa??

๐Ÿ‘‰๐ŸฟUmeshawahi kujiuliza unaipenda kwa dhati tena kutoka moyoni kazi unayoifanya??

๐Ÿ‘‰๐ŸฟUmeshawahi kujiuliza kwa nini unaomba kila Mara kuongezewa mshahara kama sio kuandamana??

๐Ÿ‘‰๐ŸฟUmeshawahi kujiuliza kwa nini unatamani ukasome uongeze elimu??

๐Ÿ‘‰๐ŸฟUmeshawahi kujiuliza kwa nini mkubwa wako kazini hataki uache kazi au ukasome au uhamie ofisi nyingine??

๐Ÿ‘‰๐ŸฟUmeshawahi kujiuliza kwa nini kila siku uko "busy" kazini au ofisini mpaka unakosa muda wa kufurahia na ndugu,jamaa,na marafiki na familia na mifuko yako au akaunti yako benki haiko "busy"??

๐Ÿ‘‰๐ŸฟUmeshawahi kujiuliza kwa nini unataka kufungua kibiashara chako au unataka ufanye kilimo Fulani kwa sababu umesikia kinawatoa watu???

๐Ÿ‘‰๐ŸฟUmeshawahi kujiuliza usipokwenda kazini kwa muda Wa wiki au mwezi au mwaka je kipato hicho hicho unachokipata utaendelea kukipata??

Hebu jiulize hayo maswali na mengine mengi yanayofanania na haya ujaribu kuona kama majibu yake unayo na kama majibu yapo ni njia gani unatumia au unategemea kutumia ili kuondokana na hayo??

Kwako wewe uliyejiajiri

๐Ÿ‘‰๐ŸฟUmeshawahi kujiuliza kwa nini biashara yako haikui kwa muda wote huo uko pale pale??

๐Ÿ‘‰๐ŸฟUmeshawahi kujiuliza kwa nini unataka uachane na hiyo biashara ufanye nyingine??

๐Ÿ‘‰๐ŸฟUmeshawahi kujiuliza kwa nini kila kitu unafanya wewe mwenyewe haumruhusu msaidizi kuwepo??

๐Ÿ‘‰๐ŸฟKwa nini huthubutu kumuachia mtu biashara yako kwa muda tu ukiondoka unafunga??

๐Ÿ‘‰๐ŸฟKwa nini unawaumiza wengine au wengine wanaumia ndipo wewe utengeneze faida yako??

๐Ÿ‘‰๐ŸฟKwa nini huwezi kuwasaidia wengine waweze kutengeneza kipato kama chako??

๐Ÿ‘‰๐ŸฟKwa nini akija mwenzako pembeni yako kufungua biashara kama yako unachukia???

๐Ÿ‘‰๐ŸฟKwa nini unachukia kulipa kodi ya pango lakini inakubidi tu ufanye hivyo??

๐Ÿ‘‰๐ŸฟNi watu wangapi wanaichukia au kuipenda biashara yako??

๐Ÿ‘‰๐ŸฟWangapi wanakuongea vizuri au vibaya kutokana na Huduma yako unayotoa??

๐Ÿ‘‰๐ŸฟKwa nini unatamani usiwe unalipa kodi??

๐Ÿ‘‰๐ŸฟKwa nini hupendi kuwaonyesha wengine njia unazotumia katika kuijenga biashara yako??ikiwa ni pamoja na upatikanaji Wa mizigo,unavyouza na unavyopata Wateja??kwa nini?

๐Ÿ‘‰๐ŸฟKwa nini hupendi kuona aliyeanza nyuma yako akifanikiwa kabla yako??

Hayo ni baadhi ya maswali ya kujiuliza wewe kama mjasiriamali au uliyejiajiri ingawa yapo na mengine unaweza kujiuliza tu uone kama utapata majibu yake na yawe ya kueleweka

โœ…
Direct PDF download

The download button now generates the PDF on the server. It no longer depends on an off-screen browser canvas, so the former blank-PDF capture path is bypassed.