ACKYSHINE ARTICLE Β· PRINTABLE READER

Madhara ya kisukari kwa nguvu za kiume

✍️ SW - Melkisedeck ShineπŸ“… April 15, 2022πŸ’¬ 0 comments
πŸ—‚οΈ Baini Siri za Kuwa na Afya Bora na Utimamu#Karibu AckySHINE#SMS, Vichekesho, Mahusiano, Biashara na Ujasiriamali, Afya, Chemsha Bongo, Dini pamoja na Vitabu kwenye PDF🌐 Kiswahili
Madhara ya kisukari kwa nguvu za kiume

Kulingana na baadhi ya chunguzi zilizofanywa na wanasayansi asilimia 60 – 70 ya wanaume hupoteza nguvu za kiume kutokana na ugonjwa wa kisukari.

Sababu ni ngumu sana kuelewa lakini hutokana na mabadiliko ya mwili ambayo hutokea baada ya mtu kupata kisukari.

Ukiachana na kupata hamu ya kufanya tendo la ndoa mara kwa mara unatakiwa kuwa na mtiririko mzuri wa damu kwenye mishipa ya uume ili uweze kusimamisha uume kwa muda mrefu.

Unahitaji mishipa ya fahamu yenye afya na pia unahitaji homoni za kiume zakutosha.

Ugonjwa wa kisukari husababisha kudhoofu kwa mishipa ya damu, misuli pamoja na mishipa ya fahamu.

Uharibifu huu hupelekea mwanaume kupoteza uwezo wa kusimamisha uume kwa muda mrefu na baadae husababisha kushindwa kusimamisha uume kabisa.

Lakini pia ugonjwa wa kisukari hupelekea maradhi ya moyo na kusababisha matatizo makubwa mwilini.

βœ…
Direct PDF download

The download button now generates the PDF on the server. It no longer depends on an off-screen browser canvas, so the former blank-PDF capture path is bypassed.