ACKYSHINE ARTICLE Β· PRINTABLE READER

Jinsi ya kupika Magimbi Kwa Nyama Ya Ng’ombe

✍️ SW - Melkisedeck ShineπŸ“… April 9, 2022πŸ’¬ 0 comments
πŸ—‚οΈ Dondoo za Mapishi na LisheπŸ—‚οΈ Upishi na Maandalizi ya Milo yenye Afya#Karibu AckySHINE🌐 Kiswahili
Jinsi ya kupika Magimbi Kwa Nyama Ya Ng’ombe

Vipimo

Majimbi (Eddoes) kiasi 6 au 7

Nyama ng’ombe Β½ kilos

Tangawizi ilosagwa 1 kijiko cha kulia

Haldi (bizari manjano/turmeric) Β½ kijiko cha chai

Tui zito la nazi vikombe 2

Chumvi kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Safisha nyama kisha weka chumvi, bizari ya manjano, tangawizi mbichi, ukaushe kwanza katika sufuria kwa kukaanga kaanga.
Ikianza kukauka, weka maji funika uchemshe iwive.
Menya majimbi ukate kate na uweke katika sufuria nyengine.
Mimina supu na nyama katika majimbi uchemshe yawive majimbi.
Mwisho weka tui zito la nazi uchanganye vizuri kisha weka katika moto kidogo tu bila kufunika yakiwa tayari.

βœ…
Direct PDF download

The download button now generates the PDF on the server. It no longer depends on an off-screen browser canvas, so the former blank-PDF capture path is bypassed.