ACKYSHINE ARTICLE Β· PRINTABLE READER

Jinsi ya kufanya nyuki waingie kwenye mzinga mpya

✍️ SW - Melkisedeck ShineπŸ“… December 26, 2020πŸ’¬ 0 comments
πŸ—‚οΈ Mbinu za Kilimo na Ufugaji Kukuongezea Mapato#Karibu AckySHINE#Makala Kuhusu Mifugo#SMS, Vichekesho, Mahusiano, Biashara na Ujasiriamali, Afya, Chemsha Bongo, Dini pamoja na Vitabu kwenye PDF#Ufugaji wa Nyuki🌐 Kiswahili
Jinsi ya kufanya nyuki waingie kwenye mzinga mpya

Ukitaka kuwavutia na kuingiza nyiki kwenye mzinga unatakiwa kufanya yafuatayo;

  1. Tafuta mahali pazuri pa-kuning’iniza mzinga wako.
  2. Weka nta kwenye mizinga yako ili kuwavutia nyuki.
  3. Hakikisha unaweka mizinga yako katika hali ya usafi na kusiwe na wadudu. Nyuki hawapendi kukaa mzinga mchafu.
  4. Hakikisha hakuna siafu wala panya wanaoishi kwenye mzinga.
  5. Ning’iniza mzinga msimu ambao kuna makundi mengi ya nyuki yanayohama. Makundi ya nyuki huama wakati ambao nyuki wamezaliana kwa wingi na kuwepo malikia mwingine kwenye mzinga hivyo kusababisha kuhama ili kuunda kundi jingine. Msimu huo wa mgawanyiko ni rahisi nyuki kufanya makazi katika mzinga wako kwa haraka. Kama haujui msimu wa makundi ya nyuki kuhama waulize wakulima wenzio wanaofuga nyuki katika eneo lako.
βœ…
Direct PDF download

The download button now generates the PDF on the server. It no longer depends on an off-screen browser canvas, so the former blank-PDF capture path is bypassed.